Hata nuru ndogo hung'aa gizani, hutia macho nuru, huonyesha njia!
Maumivu ni dalili kuwa kuna tatizo mahali fulani katika mwili wako! Fanya uchunguzi!
Maisha ni zawadi ya thamani sana tuliyopewa na Muumba wetu. Tuyatunze sana!
Pamoja tunaweza kupambana na maradhi na kuyashinda!
NASHINDWA KULALA
TUNAVYOZEEKA
MADINI YA CHUMVI
Tovuti hii imekusudia kuzungumzia masuala ya afya katika jamii zetu, kwa lugha ambayo ni nyepesi kwa wanajamii kuielewa. Nitagusia masuala ambayo nimejifunza kuwa yanarudisha nyuma sana juhudi zinazoendelea katika kuimarisha afya - hasa kuhusu maradhi sugu, ya muda mrefu au yale yanayohatarisha maisha. Baada ya kufanya kazi katika afya kwa muda usiopungua miaka 9 nimejifunza kuwa sio tu magonjwa yanayowatatiza watu wengi, ila kukosa taarifa sahihi kuhusu hali zao ndio inayozabaisha ugumu katika jitihada za kuondokana na maradhi/ matatizo hayo. Ni matumaini yangu kuwa mwanga kidogo nitakaoangaza katika tovuti hii utawafikia walengwa na kulet mabadiliko chanya katika sekta ya afya katika jamii yangu!